
Mkurugenzi wa TMA, Agnes Kijazi.
Akizungumza kwenye hafla fupi ya kufunga mafunzo ya wataalamu
katika masuala ya ukame, kilimo, mafuriko na moto wa misituni
iliyohusisha sekta mbalimbali nchini, Mkurugenzi wa TMA, Agnes Kijazi,
alisema kuwa tangu walipotoa utabiri wa hali ya hewa kwa kipindi cha
mvua za vuli (Oktoba mpaka Desemba), wameendelea kufuatilia mabadiliko
ya joto katika Bahari ya Pacifiki na kugundua joto linazidi kuongezeka
na kwa sasa limefikia nyuzi joto 2.5 juu ya wastani.
Alisema kuwa kuongezeka kwa joto magharibi mwa Bahari ya Hindi
mpaka kufikia nyuzi joto 2.0 na kupungua kwa joto mashariki mwa Bahari
ya Hindi ni wazi maeneo mengi ya nchi yatakumbwa na mvua kubwa huku
ukanda wa bahari ya Pacifiki kukitarajiwa kuwa na mvua za El- nino.
“Tunaendelea kusistiza juu ya mvua hizi kubwa ambazo zitaanza
kunyesha nchini kuanzia Oktoba, ni vizuri mamlaka husika kuanza kuchukua
hatua za kujihadhari sasa hivi tunavyoelekea kwenye msimu wa mvua,”
alisema.
Alisema kuwa TMA inawashauri watumiaji wa taarifa za hali ya hewa
wakiwamo wakulima, wafugaji na mamlaka za wanyamapori, sekta za maji na
afya watafute na kufuata ushauri wa wataalam katika sekta husika juu ya
kukabiliana na hali hiyo ya mvua kubwa inayotarajiwa nchini.
Akizungumza na washiriki 27 kutoka sekta mbalimbali waliodhurua
mafunzo hayo, Kijazi, alisema kuwa malengo ya mafunzo hayo yamefikiwa na
wahusika wayatumie katika kuboresha utendaji wao wa kazi katika taasisi
zao.
CHANZO:
NIPASHE
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni