MWAKA
huu tuna kwenda kufanya uchaguzi, miaka 20 baada ya uchaguzi wa kwanza
wa vyama vingi. Katika Uchaguzi huo Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere
alikuwa ndiyo dira elekezi ya sifa za aina ya Rais tumayemtaka kwa
wakati huo.
Oktoba 25, siku ya Uchaguzi Mkuu, tutakuwa tunatimiza miaka 16 na siku 11 ya Tanzania bila Baba wa taifa, hilo lakini halimaanishi kwamba hayupo kabisa kabisa, Mwalimu bado anaishi, yuko kwenye fikra zetu, kwenye mioyo yetu na kwa kweli kila mahali, watu aina ya Mwalimu hawafi
Hilo linajidhihirisha katika uchaguzi huu, uhai wa Mwalimu Nyerere ukoa kila mahali. Inachosikitisha hata hivyo ni matumizi mabaya ya nukuu za Mwalimu. Kila kundi hata lenye malengo ya kijahiri, ya kibaguzi na kifisadi, wantaka kutumia nukuu za Mwalimu ili tu kujipatia mradi wao.
Pamoja na kwamba watu wako watu ambao hawamkukubali, na hawajawahi kuzikubali fikra na hoja zake, hawa ghafla hugeuka vipenzi vyake wakitaka kutumia hekima zake kwa niia potofu ili wafanikishe maengo yao hata kama kwa dhati ya mioyo yao wanajua kabisa Mwalimu asigekuwa upande wao.
Wanafanya hivyo kutokana na ukweli kwamba, wanajua kwa uhakika jinsi Mwalimu Nyerere alivyoyagusa maisha ya wananchi wengi kwa aina yake ya uongozi, maisha ya kawaida aliyoishi, hata kama alikuwa ni kiongozi aliyeheshimika sana duniani, lakini bado aliishi maisha ya kitanzania, kama mwananchi wa kawaida wa Tanzania.
Katika mazingira mchanganyiko wa siasa za sasa na jinsi zinavyoonekana kuwa na ushindani mkubwa, wengi wanatamani Mwalimu angekuwepo hapa ili, kiu ya kutaka kusikia sauti yake akizugumzia sifa za aina ya kiongozi anayetakiwa, zinaashiria jambo moja tu kwamba, Nyerere ni mmoja na ataendelea kuwa mmoja.
Kama kuna mtu alikuwa na mashaka na ubaba wa taifa wa mzee huyu nadhani sasa atakubali kwa dhati kabisa kwamba taifa halina tena mzazi wake, halina mtu wa kumkimbilia linapokuwa katika msuko suko, limebaki yatima.
Mara baada ya kifo chake, kulikuwa na kauli nyingi sana za viongozi wa chama cha Mapinduzi na serikali kuwa watayalinda na kuyaenzi yote aliyoyaamini na kuyasimamia kwa kuwa hayo ndiyo hasa yaliyoifanya Tanzania iwe moja, bila ubaguzi wa rangi, dini, kabila au wa aina yeyote ile.
Wananchi walipata matumaini kwamba pamoja na kuondokewa na kiongozi, baba yao, aliyewapenda na kuwatetea kama taifa kwa nguvu zote, kulikuwa na matumaini kwamba hawa waliobaki kwa kuzingatia uzito wa maneno yao kwamba watahakikishia wanamuenzi kwa kusimamia misingi aliyoasisi.
Lakini pia tulikuwepo akina Thomaso, tusiosadiki mpaka tuone, tulikuwa na mashaka na maneno ya wasemaji hawa hasa ukizingatia mienendo yao ilivyokuwa inajieleza wazi wazi ilivyo kinyume kabisa na na ile ya Mwalimu, tulikuwa na mashaka kama kweli haya yanayosemwa yana ukweli au watu walikuwa wanasema kwa ajili ya kusema tu.
Wakati fulani niliwahi kuwaomba watu hawa wanaojiita wakereketwa wa misingi ya mwalimu na viongozi wa nchi hii wamwache mzee wetu apumzike, wasiendelee kulitukanisha jina lake kwa kujisingizia wanauenzi wakati kila kinachoendelea katika hali halisi ni kinyume kabisa na jinsi alivyotaka yeye chama na serikali viendeshwe.
Lakini bahati mbaya sana, watu hawa hawasikii wala hawakomi, wanaendelea kumfanya Mwalimu kuwa mtaji wao wa kisiasa, wanaendelea kujisingizia wanamuenzi wakati kumbe wanachokitafuta ni kujenga umaarufu na kuaminika kwa chama chao kwa jina lake lakini wakifanya mambo ambayo kwa hakika hata yeye yanamchefua.
Leo kila mahali utasikia, “Wananchi wanataka mabadiliko, wasipoyapata ndani ya CCM, watayatafuta nje ya CCM,” wanaonukuu kauli hii, hakuna mahali ambapo wanasema ni aina gani ya mabadiliko Mwalimu alikuwa anazumgumzia. Wapo watu ambao asitaka hata kuwaona lakini leo ndiyo wanaongoza kiherehere kunukuu kauli zake bila haya.
Wakati wake kiongozi alipatikana kwa hekima, busara na uadilifu wake siku hizi pesa ndiyo zinaongea zaidi, tena zile zinapatikana na kutolewa kwa njia haramu, tamaa ya kuwa rais kwa gharama yeyote imetamalaki, na uweo wa kuongoza siyo tena kigezo, leo ni una pesa nyingi kiasi gani ndiyo zinaamua, unakuwa kiongozi au la, ukiwa na za kutosha hata haijalishi wewe ni nani, kila mtu atakuwa anakuimbia nyimbo za kukusifu na kukupamba, hata umetoka jela leo, utaitwa mtakatifu wa kuigwa.
CCM yake kilikuwa chama cha wakulima na wafanyakazi, wakielezewa vyema na alama a chama jembe na nyundo, wananchi wanyonge kiliotarajia kuwakomboa toka katika minyororo ya wenye pesa na madaraka leo, chama hiki kimeambatana na wenye pesa zaidi, maskini wa Tanzania wamebaki kuwa wasindikizaji tu ndani ya chama chao, aisiye na pesa haoti hata kuwa diwani.Lakini hao hao wananukuu kauli za Mwalimu kwa maslahi yao hawawezi kuthubutu kunukuu kauli hii.
“Mtu yeyote anayeonekana anapenda sana kwenda Ikulu na hata yupo tayari kununua kura ili kumwezesha kufika Ikulu ni wa kumkwepa kama ukoma. Kwanza, hizo fedha kapata wapi. Mtanzania wa leo hawezi kununua watu bila kwanza yeye kununuliwa. Na kama kanunuliwa, atataka kuzilipaje? Kazipata wapi? Watanzania wote ni masikini tu. Mtanzania anaomba urais wetu kwa hela! Amezipata wapi? Pili, kama hajanunuliwa, kazipata wapi? Kama kakopa, atarudishaje? Ikulu pana biashara gani mtu akope mamilioni halafu aende ayalipe kwa biashara ya Ikulu? Ikulu mimi nimekaa kwa muda wa miaka ishrini na mitatu. Ikulu ni mahali pazito. Kuna biashara gani Ikulu?”
CCM nao hawachoki kutumia jina la Mwalimu na hasa kauli yake kwamba “Mimi ninang’atuka lakini naendelea kuamini kuwa bila CCM madhubuti nchi hii itayumba”. Je ni umadhubuti gani Mwalimu aliudhamiria kwa CCM, hii ya leo inaweza kujiita madhubuti?
Lakini upo kila ushahidi unaoonyesha kuwa chama hicho sasa kimetekwa na watu wenye fedha kiasi kwamba badala ya kufanya uchaguzi, siku hizi kinafanya uchuuzi wa kura, hata vijana na sura mpya zinazojitokeza katiia nafasi mbali mbali katika chaguzi zinazoendelea ni wengi wao wanatumiwa katika kile alichokieleza waziri Mkuu mstaafu Sumaye kuwa ni rushwa ya Mtandao.
Kama kweli tunataka kumuenzi baba wa taifa letu inabidi tusimame katika misngi ya haki na usawa kwa ajili ya mustakabali mwema wa taifa letu. Hatuwezi kusema eti tunamuenzi Mwalimu kwa kuigiza tu matembezi ya safari aliyofanya wakati mambo ya msingi yaliyomfanya atembee hatuyawekei mkazo wala kuyapatia umuhimu unaostahili.
Kuporomoka kwa uadilifu wa viongozi wetu katika taifa ni moja ya mambo yanayohitaji kukemewa kwa nguvu zote,na vijana huu ndio wakati wa kuonesha umuhimu wao na jinsi wao walivyo tumaini kwa taifa lao.
Ofisi za umma sasa zimekuwa aina fulani ya miradi ya uhakika ya kuweza kumtajirisha mtu ghafla, nafasi za uongozi wa kisiasa ndio usiseme, watu wanawekeza mamilioni ya pesa katika chaguzi ili washinde wakijua wazi kwamba baada ya ushindi, inakuwa zamu yao kuchuma na kuneemeka kwa gharama ya umaskini wa Tanzania na watu wake.
Katikati ya haya wapo watu wanaimba usiku kucha wanataka tuwasadiki kwamba wanamuenzi baba wa taifa na misingi aliyoisimika na uadilifu na uongozi wa utumishi kwa umma. Taifa leo linalia na kunyong’onyea kwa kukosa aina ya viongozi ambao ni watumishi wa umma (servant leader).
Viongozi wetu leo, hata wale ambao nafasi zao ni za uwakilishi wa wananchi, ni viongozi wa kutumikiwa, wanakaa kutengeneza taifa la kuwanufaisha wachache na kuwaacha wengne wengi ambao kimsingi ndio wenye nchi, wanawaya waya na umaskini wa kutupwa.
Kama ni lazima taifa hili liondokane na madhira yanayolikabili sasa wenye wajibu wa kulikomboa taifa toka katika hali hiyo ni vijana wa taifa hili, lakini hata wao hawawezi kutimiza wajibu wao huo wa msingi kama wenyewe kwanza hawajikomboi na kuachana na siasa za maslahi binafsi.
Si busara sana kutmia jina la Mwalimu kinafika, wengine wetu tunaomuheshimu tunaona ni vyema akaachwa apumzike kwa amani kwa kuwa, kwa unafiki unaozunguka kukaririwa kwa jina lake, tunamkosesha amani mzee wetu huyo.
Imeandikwa na Ng'wandu Bruno

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni