Jumamosi, Septemba 12, 2015

Jifunze Kuimba na Joett Vocal Training CD Introduction Video #2

Kreni yaua 107 mjini Mecca

Gavana katika eneo la Mecca ameamrisha kufanyika uchunguzi kufuatia kuanguka kwa kreni katika msikiti mkubwa zaidi duniani.Utawala nchini Saudi Arabia unasema kuwa upepo mkali ndio ulisababisha kreni iliyokuwa ikitumika kwa ujenzi kuanguka kwa msikiti mkubwa mjini mecca ambapo watu 107 waliuawa na wengine takriban 200 kujeruhiwa.

Mkuu wa idara ya ulinzi wa angani nchini humo alisema kuwa kulikuwa na mvua kubwa wakati ajali hiyo ilipotokea na upepo ulikuwa ukivuma kwa takriban kilomita 83 kwa saa.
Msikiti huo unazunguka eneo takatifu la kiislamu la Kaaba na ndio msikiti mkubwa zaidi duniani na huwavutia mamia ya waislamu ambao huenda kuhiji kila mwaka.
Karibu watu milioni moja wamewasili nchini Saudi Arabia kabla ya sherehe za mwaka huu ambazo zinaanza wiki mbili zinazokuja.
kreni iliyokuwa ikitumika kwa ujenzi kuanguka kwa msikiti mkubwa mjini Mecca ambapo watu 107

Mamlaka ya hali ya hewa yatoa angalizo.


Mkurugenzi wa TMA, Agnes Kijazi.
Mamlaka ya hali ya hewa nchini (TMA) imesisitiza kuwapo kwa mvua kubwa katika maeneo mengi ya nchi na kuzitaka mamlaka husika kuanza kuchukua tahadhari mapema.
Akizungumza kwenye hafla fupi ya kufunga mafunzo ya wataalamu katika masuala ya ukame, kilimo, mafuriko na moto wa misituni iliyohusisha sekta mbalimbali nchini, Mkurugenzi wa TMA, Agnes Kijazi, alisema kuwa tangu walipotoa utabiri wa hali ya hewa kwa kipindi cha mvua za vuli (Oktoba mpaka Desemba), wameendelea kufuatilia mabadiliko ya joto katika Bahari ya Pacifiki na kugundua joto linazidi kuongezeka na kwa sasa limefikia nyuzi joto 2.5 juu ya wastani.
Alisema kuwa kuongezeka kwa joto magharibi mwa Bahari ya Hindi mpaka kufikia nyuzi joto 2.0 na kupungua kwa joto mashariki mwa Bahari ya Hindi ni wazi maeneo mengi ya nchi yatakumbwa na mvua kubwa huku ukanda wa bahari ya Pacifiki kukitarajiwa kuwa na mvua za El- nino.

Nafasi za masomo Pre - form one!


MWALIMU OPEN SCHOOL CENTER
0755 680 878
0713 025 340

 
www.facebook.com/GeofreyNgunya
 http://ngunya.blogspot.com/

Tunawakaribisha wahitimu wote wa darasa la saba kwenye masomo ya  
 PRE-FORM ONE 
yatakayo anza tarehe 14/09/2015 kwa miezi mitatu (3) mpaka tarehe  19/12/2015.
kwa masomo ya kiingereza, Kiswahili, Hisabati na masomo ya sayansi kwa vitendo.

Mwanafunzi wote watapatia vitu vifuatavyo bure:
 


(1)Peni. 

(2)Daftari.

(3)Kutalii maeneo mbalimbali kwa ajili ya kujifunza zaidi kwa vitendo ndani na nje ya Manispaa ya Morogoro.

(4)T - shirt moja sare ya shule.
 
NB;Wahi kuchukua fomu mapema nafasi ni chache tunahitaji wanafunzi 50 tunapatikana Morogoro mjini maeneo ya Oilcom nane nane tunatazamana na ALFAGEMS sekondari school au piga simu zetu zilizopo hapo juu.

WOTE MNAKARIBISHWA 

Wanasiasa kuna maisha zaidi baada ya uchaguzi-Mwamalanga


Wiki hii Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, ameibuka ndani ya vyombo vya habari ‘kumpopoa’ Katibu Mkuu wa Chadema, aliyejiondoa kwenye siasa kwa madai ya kupinga ujio wa Edward Lowassa ndani ya chama hicho. Hata hivyo Askofu Gwajima anampinga kuwa kilichomuondoa Chadema ni kupingwa na mchumba wake, aliyetaka awe rais naye apewe heshima ya mama wa Ikulu .
Kiongozi huyo wa kiroho, ameibua mambo mengi ambayo wapo wanaounga mkono hatua hiyo lakini kuna baadhi wanaoitafsiri kwa kuipa sura ya kidunia na si kiroho maana pengine kama kiongozi wa imani asingefanya hivyo. Pamoja na hisia hizo viongozi wenzake wa kiroho wanasema kutoka kwa ‘waraka wa Gwajima’ kuna cha kujifunza kama anavyoeleza Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kipentekoste, William Mwamalanga. (Pichani).

Jumanne, Septemba 08, 2015

Nafasi za masomo!

MWALIMU OPEN SCHOOL CENTER
0755 680 878
0713 025 340

 
www.facebook.com/GeofreyNgunya
 http://ngunya.blogspot.com/

Tunawakaribisha wahitimu wote wa darasa la saba kwenye masomo ya  
 PRE-FORM ONE 
yatakayo anza tarehe 14/09/2015 kwa miezi mitatu (3) mpaka tarehe  19/12/2015.
kwa masomo ya kiingereza, Kiswahili, Hisabati na masomo ya sayansi kwa vitendo.

Mwanafunzi wote watapatia vitu vifuatavyo bure:
 


(1)Peni. 

(2)Daftari.

(3)Kutalii maeneo mbalimbali kwa ajili ya kujifunza zaidi kwa vitendo ndani na nje ya Manispaa ya Morogoro.

(4)T - shirt moja sare ya shule.
 
NB;Wahi kuchukua fomu mapema nafasi ni chache tunahitaji wanafunzi 50 tunapatikana Morogoro mjini maeneo ya Oilcom nane nane tunatazamana na ALFAGEMS sekondari school au piga simu zetu zilizopo hapo juu.

WOTE MNAKARIBISHWA 

Tanzania Presidential Debate (Swahili students in USA)

Tanesco hamjatenda haki, mngetoa taarifa mapema.


Shirika la Umeme nchini (Tanesco), juzi lilitangazia umma kwamba nchi nzima itakuwa gizani kwa takriban wiki nzima kuanzia jana.
Shirika hilo lilieleza kuwa hali hiyo inatokana na kuzimwa kwa mitambo ya gesi inayozalisha umeme kutoka Songosongo mkoani Lindi.
Tanesco ilifafanua kuwa imechukua hatua hiyo kutokana na kazi ya kuunganisha bomba la gesi kutoka Mtwara na mtambo wa umeme wa Kinyerezi II.
Aidha, hali ya umeme ilitarajiwa kuwa mbaya zaidi jana kwa kuwa mitambo yote ya kuzalisha nishati hiyo ilikuwa inatarajiwa kuzimwa ili kufanikisha kazi hiyo.
Tunaamini kwamba dhamira ya Tanesco ni njema na imelenga kuboresha utoaji huduma umeme nchini ambayo kwa miaka nenda rudi, imekuwa haikidhi matarajio ya wateja wake na Watanzania kwa ujumla.